Waziri Rice kukutana na Rais Abbas
5 Novemba 2007Matangazo
Siku ya Jumapili,Rice alikuwa na majadiliano pamoja na viongozi wa Kiisraeli katika jitahada ya kuendeleza mpango wa kuunda taifa la Palestina.Amesema,
„Machafuko ya itikadi kali kimsingi yamezindua mkakati wa mfungamano mpya katika Mashariki ya Kati.Mataifa yenye kuwajibika ambayo hapo awali yalikuwa mahasimu,sasa yameona kuwa maslahi yao labda ni moja-kupambana na kitisho cha aina moja.Pia taifa la Palestina lenye siasa za wastani ni kinga dhidi ya kitisho hicho.“
Kwa upande mwingine Waziri wa Nje wa Israel,Tzipi Livni amemuambia waziri mwenzake Rice kuwa Israel haitotekeleza mpango wo wote utakaopendekezwa na Marekani,kabla ya kuhakikishiwa usalama wake.