1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
UchumiChina

Waziri wa Fedha wa Marekani kujadiliana ´mazito´ na China

5 Aprili 2024

Waziri wa Fedha wa Marekani Janet Yellen anayeitembelea China anatarajiwa hii leo Ijumaa kuanza mazungumzo mazito ya siku nne na maafisa wa nchi hiyo.

Waziri wa Fedha wa Marekani Janet Yellen akiwasili China
Waziri wa Fedha wa Marekani Janet Yellen akiwasili China Picha: Andy Wong/AP/picture alliance

Mazungumzo hayo yatajikita juu ya uzalishaji uliopindukia viwango wa viwanda vya China na mazingira magumu ya ushindani yanayozikabili kampuni za biashara za Marekani.

Yellen aliwasili siku ya Alhamisi kwenye mji wenye shughuli nyingi za biashara wa Guangzhou na hii leo amepangiwa kukutana na gavana wa jimbo la Guangdong uliko mji huo pamoja na Naibu Waziri Mkuu wa China, He Lifeng.

Huo ni mwendelezo wa jitihada za pande hizo mbili za kupunguza mivutano kwenye maeneo yote muhimu husasani biashara na masuala ya kijeshi.

Utawala wa rais Joe Biden unatiwa wasiwasi na uzalishaji wa kupita kiasi unaofanywa na makampuni ya China hasa kwenye uundaji wa vyombo na vifaa vya kielektroniki vinavyoliemea soko la dunia.

Yellen analenga kuwaambia maafisa wa China kuwa uzalishaji wa aina hiyo unayaumiza makampuni ya Marekani na nchi nyingine duniani na pia siyo rafiki kwa hatma ya viwanda vya nchi China.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW