1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Migogoro

Waziri wa Israel akosoa uwepo wa kikosi cha UNIFIL Lebanon

14 Oktoba 2024

Waziri wa nishati wa Israel Eli Cohen ameulaumu ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Lebanon.

Waziri wa nishati wa Israel Eli Cohen.
Waziri wa nishati wa Israel Eli Cohen.Picha: Eli Cohen (@elicoh1)/X

Waziri wa nishati wa Israel Eli Cohen ameulaumu ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Lebanon, UNIFIL kwa kusema "hakina maana" na kwamba kimeshindwa kuwalinda Waisraeli kutokana na mashambulizi ya Hezbollah.

Kupitia mtandao wa kijamii wa X Cohen ametoa wito wa ujumbe huo kujiondoa huku mapigano yakizidi kuongezeka.

Mashariki ya Kati, wakati huo huo, bado iko katika hali ya tahadhari kwa Israel kulipiza kisasi dhidi ya Iran kwa shambulizi la Oktoba 1 la makombora ya masafa marefu kujibu mashambulizi ya Israel dhidi ya Lebanon.

Haya yanajiri huku Marekani ikisema itatuma wanajeshi wake nchini Israel pamoja na mfumo wa hali ya juu wa kupambana na makombora, wakati Israel ikizingatia kulipiza kisasi kinachotarajiwa dhidi ya Iran.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW