1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waziri wa Israel amshtumu meya mpya wa New York

5 Novemba 2025

Waziri wa Israel anayehusika na maslahi ya Waisraeli wanaoishi ughaibuni Amichai Chikli, leo amemshtumu meya mteule wa New York Zohran Mamdani na kumtaja kuwa "mfuasi wa kundi la Hamas."

Marekani, New York 2025 |  Zohran Mamdani akihutubia waandishi wa habari
Meya mteule wa New York, Zohran MamdaniPicha: Kylie Cooper/REUTERS

Kupitia chapisho kwenye mtandao wa X, Chikli amesema mji huo ambao awali ulikuwa ishara ya uhuru wa kimataifa umekabidhi funguo zake kwa wafuasi wa Hamas.

Chikli pia amesema New York haitakuwa tena kama ilivyokuwa awali hasa kwa jamii ya Kiyahudi na akaongeza kuwa jiji hilo linajitumbukiza wazi ndani ya shimo ambalo Uingereza tayari imejiingiza.

Ameendelea kusema kwamba maoni ya Mamdani hayatofautiani pakubwa na yale ya wafuasi wa itikadi kali ambao, miaka 25 iliyopita, waliwaua watu elfu tatu, akimaanisha mashambulizi ya Septemba 11, 2001 yaliofanywa na kundi la Al-Qaeda huko New York na Washington.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW