Svenja Schulze afanya ziara Mashariki ya Kati
19 Desemba 2023Matangazo
Waziri Schulze anatarajiwa kukutana na wawakilishi wa asasi ya kiraia ya nchini Israel pamoja na watu walioathirika kutokana na shambulio la Hamas la tarehe 7 mwezi Oktoba.
Waziri huyo wa Ujerumani pia atafanya mazungumzo na wakaazi wa mji wa Kibbutz ulio karibu na mpaka wa Gaza.
Israel yaendeleza mashambulizi Gaza huku miito ya usitishwaji vita ikitolewa
Baadaye, Waziri Schulze atakutana na Waziri Mkuu wa Palestina, Mohammad Shtayyeh, na pia atatembelea kambi ya wakimbizi ya Al-Amari iliyopo kwenye Ukingo wa Magharibi, ambako atakutana na wawakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Misaada na Kazi kwa Wapalestina (UNRWA).