Waziri wa Maendeleo wa Ujerumani alizwa na hali ya Sudan
28 Novemba 2024Katika mahojiano maalumu na DW Afrika, Schulze alielezea hali ilivyo kwenye mpaka wa Sudan na Chad, ambako maelfu ya wakimbizi, hasa wanawake na watoto, wamekimbia machafuko.
Ameisifu Chad kwa mshikamano wake licha ya kuwa moja ya nchi masikini zaidi, na kuuhimiza ulimwengu kuchukua hatua.
Soma pia: Waziri wa Ujerumani atahadharisha juu ya ushawishi wa Urusi barani Afrika
Schulze pia amebainisha kuwa mgogoro huo umepuuzwa kutokana na migogoro ya Mashariki ya Kati na Ukraine, akitoa wito kwa uhamasishaji mkubwa wa kimataifa na shinikizo kwa pande husika.
Amekariri msimamo wa Ujerumani wa kuzuia silaha kufika kwenye mgogoro huo na kusisitiza umuhimu wa ushirikiano wa kimataifa, hasa na Umoja wa Afrika, kukabiliana na mgogoro huo wakati Marekani inapojiondoa kwenye dhima yake ya jadi.