1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waziri wa Maendeleo wa Ujerumani Schulze, aitembelea Syria

15 Januari 2025

Waziri wa Maendeleo wa Ujerumani Svenja Schulze, amekwenda Syria leo Jumatano kuunga mkono miradi inayotokana na msaada uliotolewa kwa taifa hilo lililoharibiwa na vita.

Syria | Waziri wa Maendeleo Schulze azuru Damascus
Syria | Waziri wa Maendeleo Schulze azuru DamascusPicha: Sebastian Gollnow/dpa/picture alliance

Ujerumani inasaidia mfumo wa afya wa Syria kupitia ushirikiano kati ya hospitali za Syria na Ujerumani, Waziri wa Maendeleo Svenja Schulze alisema wakati wa ziara yake mjini Damascus Jumatano. Schulze alikutana na madaktari wa Syria pamoja na waziri wa afya wa serikali ya mpito, Maher al-Sharaa, ambaye pia ni daktari na kaka wa kiongozi wa serikali hiyo, Ahmed al-Sharaa.

Wizara ya Maendeleo ya Ujerumani inaona changamoto kubwa katika mfumo wa afya wa Syria, ambao kihistoria umekuwa imara sana. Madaktari kutoka Ujerumani wanatarajiwa kusafiri kwenda Syria kutoa mafunzo au kufanya mazoezi ya kutumia vifaa vipya pamoja na wenzao wa huko, huku kozi za mafunzo nchini Ujerumani pia zikiwa sehemu ya mpango huo.

Soma pia: Ulaya, Arabuni wakutana kuijadili Syria

Mashambulizi ya kimakusudi dhidi ya hospitali yaliyofanywa na vikosi vya aliyekuwa mtawala wa Syria, Bashar al-Assad, wakati wa vita vya muda mrefu na vya kikatili vya wenyewe kwa wenyewe, pamoja na kukimbia kwa madaktari na wauguzi wengi waliobobea kwenda nje ya nchi, kumesababisha pengo kubwa katika sekta ya afya.

Selfie na Merkel yampa Umaarufu

02:08

This browser does not support the video element.

Kwa mujibu wa Wizara ya Maendeleo ya Ujerumani, zaidi ya nusu ya wafanyakazi wa sekta ya afya ya Syria wameondoka nchini. Takriban madaktari 5,800 na wauguzi 2,000 wenye pasipoti za Syria wanahudumu nchini Ujerumani pekee, kwa mujibu wa takwimu za serikali, na madaktari wengi waliozaliwa Syria tayari wamepewa uraia wa Ujerumani.

Iyad Durmus, daktari wa macho wa Kijerumani mwenye asili ya Syria aliyehamia Ujerumani kama mwanafunzi wa udaktari mwaka 2005, anaambatana na Schulze katika ziara hiyo. Alisema kwamba idadi kubwa ya madaktari wa Syria wamekuwa wakingoja kwa miaka bila mafanikio kutambuliwa kwa vyeti vyao nchini Ujerumani: "Natarajia kwamba wengi wa watu hawa watarudi."

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW