Waziri wa mambo ya kigeni wa Kenya kuizuru Urusi
11 Februari 2026
Matangazo
Mudavadi amesema kuwa katika ziara yake hiyo, atafuatilia na kuhakikisha kuachiwa kwa Wakenya wanaoshikiliwa kama wafungwa wa kivita nchini Ukraine na kufahamu pia hali ya wale walio mahospitalini.
Waziri huyo amesema zaidi ya Wakenya 30 wamerejeshwa nyumbani kutoka Urusi katika kipindi cha siku miezi miwili iliyopita na mashirika feki ya ajira kufungwa katika nchi hiyo ya Afrika Mashariki.
"Ombi letu kwa serikali ya Urusi ni kuhakikisha Wakenya hawako katika orodha ya wanaotarajiwa kusajiliwa. Tunataka hilo liwe wazi kabisa," alisema Mudavadi.
Ripoti katika wiki kadhaa zilizopita zinaonesha kuwa Wakenya waliolaghaiwa kwenda Urusi kufanya kazi zenye malipo ya juu, wanafariki dunia katika uwanja wa mapambano na kupata majeraha mabaya.