1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waziri wa mambo ya kigeni wa Urusi yuko ziarani Cairo

16 Septemba 2024

Waziri wa mambo ya nje wa Urusi,Sergei Lavrov ameishutumu Marekani kwa kuyawekea kigingi maazimio ya baraza la usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu makubaliano ya usitishaji vita Gaza kati ya Israel na Hamas.

Sergei Lawrow
Waziri wa Mambo ya nje wa Urusi Sergei Lavrov.Picha: Russian Foreign Ministry/Handout via REUTERS

Mwanadiplomasia huyo wa ngazi za juu wa Urusi akizungumza baada ya mazungumzo yake na mwenzake wa Misri Badr Abdelatty,mjini Cairo, amesema Urusi inakaribisha juhudi za kushinikiza kufikiwa makubaliano ya kusitisha vita vilivyodumu miezi 11.

Ameishutumu Marekani akisema nchi hiyo haitaki kupitisha maamuzi yoyote yanayoungwa mkono na kila mtu,kumaliza vita Gaza.

Soma pia: Israel na Misri zaruhusu misaada ya kibinaadamu kupelekwa Gaza

"Na kama maazimio ya baraza la usalama la Umoja wa Mataifa,kuhusu vita kati ya Israel na Hamas katika Gaza yalivyopitishwa bila ya mwafaka,hivyo ndivyo yalivyobakia hadi hivi sasa. Hakuna ahadi za Marekani zilizotimizwa. Lakini haimaanishi kwamba tunapaswa kuziachia hapo juhudi zetu," alsiema Lavrov.

Mbio za Palestina kufuzu Kombe la Dunia zitafikia wapi?

01:16

This browser does not support the video element.

Kundi la Hamas linataka yawepo makubaliano ya kudumu ya usitishaji vita na kuondoka kikamilifu kwa vikosi vya Israel kutoka Gaza kama sehemu ya makubaliano ya kuwaachia huru mateka raia wa Israel inayowashikilia.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW