1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUingereza

Suella Braverman atarajiwa kufanya ziara nchini Marekani

24 Septemba 2023

Waziri wa mambo ya ndani wa Uingereza Suella Braverman anatarajia wiki hii kuanza ziara ya siku tatu nchini Marekani ambako atazungumzia shinikizo kubwa linalosababishwa na uhamiaji haramu

Waziri wa mambo ya ndani wa Uingereza Suella Braverman
Waziri wa mambo ya ndani wa Uingereza Suella BravermanPicha: Kin Cheung/AP/dpa/picture alliance

Braverman anatarajiwa kuwasilisha muongozo kuhusu jinsi mataifa yanaweza kukabiliana na mzozo wa uhamiaji haramu na kuangazia jinsi Uingereza imekuwa kinara katika kuleta mbinu za ubunifu kushughulikia suala hilo.

Soma pia:EU agency agrees to help Athens deport more migrants

Braverman amesema uhamiaji haramu na harakati za kuhama kwa watu wengi kote ulimwenguni ambazo hazijawahi kutokea, zinaweka shinikizo kali kwa Marekani, Uingereza na Ulaya.

Braverman kufanya mazungumzo na maafisa wakuu wa Marekani

Braverman, ambaye atasafiri kuelekea Marekani kesho Jumatatu, atatafuta ushirikiano wa karibu na nchi hiyo katika kushughulikia uhamiaji haramu na uhalifu wa vikundi vya kuratibu uhamiaji. Katika ziara hiyo,  Braveman atafanya mazungumzo na wabunge pamoja na maafisa wakuu wa Marekani.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW