Umoja wa Ulaya wataka kuwalinda zaidi wakimbizi wa Ukraine
15 Septemba 2023Matangazo
Nancy Faeser ameyasema hayo katika mahojiano yaliyochapishwa leo kwenye magazeti ya Ujerumani ya shirika la Funke Mediengruppe.
Waziri huyo wa mambo ya ndani wa Ujerumani ameeleza kuwa, hivi karibuni atajadili juu ya suala hilo na mawaziri wengine wa mambo ya ndani wa Umoja wa Ulaya.
Mnamo siku ya Jumatano, Rais wa Halmashauri Kuu ya Umoja wa Ulaya Ursula von der Leyen alipendekeza kuongeza muda wa hadhi ya ulinzi ndani ya Umoja wa Ulaya kwa wakimbizi wa Ukraine.
Mataifa ya Umoja wa Ulaya yaliamua kuwapa hadhi maalum raia wa Ukraine wanaotafuta hifadhi ndani ya EU kufuatia uvamizi kamili wa Urusi mnamo Februari, mwaka 2022.