Waziri wa mambo ya nje wa Afghanistan afanya ziara Pakistan.
6 Mei 2023Baada ya mkutano wa mapema wiki hii wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres na wajumbe wa nchi kadhaa kuijadili Afghanistan katika mji wa Doha nchini Qatar, waziri wa mambo ya nje wa serikali ya Taliban nchini Afghanistan, ambayo haitambuliwi kimataifa, anafanya mazungumzo leo Jumamosi na wenzake kutoka Pakistan na China. Waziri huyo Amir Khan Muttaqi aliyewekewa vikwazo vya kimataifa vinavyomnyima ruhusa ya kuondoka Afghanistan amefanya ziara ya nadra baada ya kuruhusiwa kuzuru mji mkuu wa Pakistan, Islamabad. China na Pakistan ni majirani muhimu wa Afghanistan. China na nchi hiyo zimegawanywa na mpaka wa pamoja wenye rasilimali kubwa za madini na kwa upande wa Pakistan nchi hiyo na Afghanistan zinagawanywa na mpaka mrefu ambao Pakistan ndio macho ya kulinda usalama kwenye mpaka huo.