1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaChina

Waziri wa mambo ya nje wa China aanza ziara yake Marekani

26 Oktoba 2023

Ziara hii inakuja wakati ambapo Marekani na China zinatafuta njia ya kusuluhisha tofauti zao za kimkakati na kufungua njia ya mkutano wa kilele unaotarajiwa kati ya Rais Joe Biden na mwenzake Xi Jinping.

Russland Sankt Petersburg | Treffen zwischen Präsident Putin und dem chinesischen Außenminister Wang Yi
Picha: Sputnik/Mikhail Metzel/REUTERS

Ziara hii inakuja wakati ambapo Marekani na China zinatafuta njia ya kusuluhisha tofauti zao za kimkakati na kufungua njia ya mkutano wa kilele unaotarajiwa kati ya Rais Joe Biden na mwenzake Xi Jinping.

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken atampokea Wang na hapo juzi Jumanne aliliambia Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwamba atashirikiana naye ili kuzuia mgogoro wa Mashariki ya Kati kuenea.

Marekani inatarajia kwamba China inaweza kutumia ushawishi wake na Iran kuzuia hilo. Wachambuzi lakini hawatarajii matokeo ya haraka kutokana na mkutano wa wanadiplomasia hao wakuu, licha ya Beijing na Washington wote kuzungumzia kutafuta maeneo wanayoweza kushirikiana.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW