SiasaChina
Waziri wa mambo ya nje wa China kuzuru nchi za Afrika
3 Januari 2025Matangazo
Taarifa hiyo imetolewa leo na wizara ya mambo ya nje ya China. Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China, Mao Ning, amesema ziara hiyo itafikisha mwaka wa 35 mfululizo kwa waziri wa masuala ya kigeni wa China kuzuru nchi za bara la Afrika, katika ziara yake ya kwanza nchi za nje mwanzoni mwa mwaka. Mwaka 2024, Wang alizitembelea Tunisia, Togo na Ivory Coast.