Choe Son Hui, kufanya ziara fupi Urusi
29 Oktoba 2024Matangazo
Waziri Choe Son anafanya ziara hiyo katika muktadha wa tuhuma juu ya nchi yake kutaka kuingia katika vita vya Urusi na Ukraine.
Jumuiya ya kijeshi ya NATO, Korea Kusini na Marekani zimeungana katika kuthibitisha kuwa Korea Kaskazini imepeleka wanajeshi nchini Urusi.
NATO imesema vikosi vya jeshi la Korea Kaskazini vilipelekwa katika eneo la Urusi la Kursk kwenye mpaka na Ukraine.
Waziri wa Mambo ya nje wa Korea Kaskazini azuru Moscow
Wizara ya Ulinzi ya Marekani imesema Marekani haitaweka vizuizi vipya kwa Ukraine kutumia silaha za Marekani ikiwa Korea Kaskazini itaingia katika vita vya Urusi dhidi ya Ukraine.
Wizara ya Ulinzi ya Marekani, Pentagon, inadai kuwa Korea Kaskazini imepeleka askari 10,000 mashariki mwa Urusi kwa ajili ya mafunzo.