1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUrusi

Waziri wa Mambo ya nje wa Korea Kaskazini azuru Moscow

15 Januari 2024

Urusi imesema inajenga mahusiano na mshirika wake Korea Kaskazini katika nyanja zote.

Hofu ya kimataifa inaendelea kuongezeka kuhusiana na madai ya kuwepo ushirikiano wa mpango wa silaha kati ya Korea Kaskazini na Urusi.
Hofu ya kimataifa inaendelea kuongezeka kuhusiana na madai ya kuwepo ushirikiano wa mpango wa silaha kati ya Korea Kaskazini na Urusi.Picha: Russian Foreign Ministry/REUTERS

Msemaji wa Ikulu ya Kremlin Dmytry Peskov ameyasema hayo wakati Waziri wa Mambo ya Nje wa Korea Kaskazini Choe Son Hui akianza ziara yake mjini Moscow.

Amesema makubaliano yaliyofikiwa kati ya Rais wa Urusi Vladmir Putin na Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un wakati walikutana mwaka jana katika uzinduzi wa satelaiti ya Urusi, yatajadiliwa wakati wa ziara ya Choe ya siku tatu.

Hofu ya kimataifa inaendelea kuongezeka kuhusiana na madai ya kuwepo ushirikiano wa mpango wa silaha kati ya Korea Kaskazini na Urusi.

Marekani na Korea Kusini zinasema Korea Kaskazini imeiuzia Urusi silaha, yakiwemo makombora, ili kuisaidia katika vita vyake nchini Ukraine.

Serikali ya Biden inasema ina ushahidi kuwa makombora yaliyotolewa na Korea Kaskazini kwa Urusi yametumika nchini Ukraine.