1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Antony Blinken atarajiwa kuwasili Moldova

29 Mei 2024

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken anatarajiwa kuwasili Chisinau, mji mkuu wa Moldova,ambako ni kituo cha kwanza cha ziara yake fupi barani Ulaya.

Antony Blinken
Waziri wa ammbo ya nchi za nje wa Marekani Antony BlinkenPicha: Brendan Smialowski/REUTERS

Katika ziara hiyo atakutana na rais Maia Sandu na analenga kuimarisha uungaji mkono wa nchi za Magharibi kwa Ukraine katika mataifa yote washirika wa Jumuiya ya kujihami ya NATO na mataifa jirani.

Ziara hiyo inakuja wakati Ukraine ikijaribu kuzuia mashambulizi yaliyoongezeka ya Urusi kwenye maeneo ya mashariki mwa nchi hiyo, huku rais Vladmir Putin akizionya nchi za Magharibi kwamba  kuiruhusu Ukraine kutumia silaha za mataifa hayo  kushambulia ndani ya ardhi yake ni hatua inayoweza kuchochea vita vya dunia.

Ukraine imesema Urusi inazidisha mashambulizi nchini humo

Baadae wiki hii atakwenda Prague kushiriki mkutano usiokuwa rasmi wa mawaziri wa mambo ya nje wa nchi wanachama wa  NATO wa maandalizi ya mkutano wa kilele wa viongozi wakuu utakaofanyika Julai.
 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW