1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUfaransa

Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa kufanya ziara Afrika

20 Machi 2024

Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa Stéphane Séjourné, anatazamiwa mwezi ujao kuanza ziara yake ya kwanza katika nchi tatu za Afrika ambazo ni Rwanda, Kenya na Ivory Coast.

Ufaransa Paris 2024 | Waziri wa mambo ya nje Stephane Sejourne
Waziri wa mambo ya nje wa Ufaransa Stephane SejournePicha: Thomas Padilla/REUTERS

Hii inatokana na juhudi za serikali ya Ufaransa kujaribu kuimarisha mahusiano yake na nchi za Afrika baada ya kupata misukosuko katika kanda ya Sahel. 

Ziara hiyo ya Waziri Séjourné iliyopangwa kuanzia tarehe 6 hadi 9 Aprili, itaanzia nchini Kenya ambapo atajadili jinsi ya kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi, kiutamaduni na kitaaluma.

Baadaye ataendelea na safari yake hadi nchini Rwanda ambapo ataiwakilisha Ufaransa katika kumbukumbu za mauaji ya halaiki ya mwaka 1994 ambapo watu zaidi ya 800,000 wameuawa wengi wao wakiwa ni jamii ya walio wachache ya Watutsi. Ziara ya Séjourné itahitimishwa nchini Ivory Coast ambayo imekuwa mshirika wa muda mrefu wa Ufaransa.

Kwa habari nyingine za Afrika, karibu kwenye chaneli yetu ya YouTube. 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW