1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Maas, ziarani Afrika

Sylvia Mwehozi
3 Septemba 2019

Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Heiko Maas, ameanza ziara ya siku nne barani Afrika huku Sudan ikiwa nchi mojawapo atakayotembelea.

Deutschland Flughafen Tegel in Berlin | Heiko Maas, Außenminister | Hintergrund: defekter Airbus A319
Picha: picture-alliance/dpa/K. Nietfeld

Maas anakuwa mwanadiplomasia wa kwanza wa ngazi ya juu wa Ulaya kukutana na uongozi mpya wa nchi hiyo. Maas amesema kwamba Sudan ipo katika mabadiliko ya kihistoria na kwamba wanataka kuunga mkono uongozi mpya katika jukumu zito la kuifungua milango ya nchi, kufanya mageuzi na maandalizi ya uchaguzi wa kidemokrasia. Aidha ameongeza kwamba huu ni wakati wa Sudan kutumia nafasi hiyo, kupokea uungwaji mkono kutoka Jumuiya za kimataifa. Maas ataitembelea pia Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Jumanne jioni, ambapo miongoni mwa mambo mengine, atapata taarifa za ujumbe wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa MONUSCO pamoja na mapambano dhidi ya ugonjwa wa mripuko wa ebola. Maas ataitembelea Kivu ya Kaskazini ambayo imeathiriwa vibaya na ugonjwa huo.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW