1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wadephul ziarani Syria kuimarisha ushirikiano

30 Oktoba 2025

Rais wa Syria Ahmed al-Sharaa amekutana leo na kufanya mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Ujerumani Johann Wadephul katika juhudi za kuimarisha ushirikiano kati ya nchi hizo mbili.

Damascus, Syria
Waziri wa mambo ya kigeni Johann Wadephul alipowasili Syria 30.10.2025Picha: Marcus Brandt/dpa/picture alliance

Ni katika ziara ya kwanza ya Wadephul nchini Syria baada ya ziara mbili za mtangulizi wake Annalena Baerbock ambaye mwezi Machi alifungua ubalozi wa Ujerumani mjini Damascus.

Ushirikiano wa kisiasa, uchumi na masuala ya kiutu kuimarishwa

Taarifa iliyotolewa na wizara ya mambo ya nje ya Ujerumani imesema mazungumzo hayo yanalenga kuimarisha ushirikiano wa kisiasa, kiuchumi na masuala ya kiutu.

Itakumbukwa kuwa Ujerumani iliwapokea maelfu ya wakimbizi kutoka Syria wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe kwa kipindi cha miaka 14.  Akiwa na ujumbe wake, Wadephul anatarajiwa kuelekea Lebanon na Bahrain katika ziara yake Mashariki ya Kati.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW