1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUkraine

Waziri wa Mambo ya Nje wa Ukraine kuelekea India wiki ijayo

20 Machi 2024

Waziri wa Mambo ya Nje wa Ukraine Dmytro Kuleba, anatazamiwa kufanya ziara nchini India wiki ijayo.

Ujerumani I Heiko Maas akutana na waziri wa mambo ya nje wa Ukraine, Dmytro Kuleba
Waziri wa mambo ya nje wa Ukraine Dmytro KulebaPicha: John Macdougall/AP/picture alliance

Haya yanafanyika wakati ambapo Kyiv inatafuta uungwaji mkono zaidi katika mpango wake wa amani unaotaka kuondolewa kwa vikosi vya Urusi na uheshimishaji wa mipaka ya Ukraine.

Hii ni ziara ya kwanza kabisa ya Kuleba nchini India tangu Urusi ilipoivamia Ukraine miaka miwili iliyopita.

New Delhi, ambayo imekuwa na mahusiano ya karibu ya kiuchumi na kiulinzi na Moscow, hadi sasa imekataa kuikosoa Urusi kwa uvamizi wake nchii Ukraine na badala yake imezidisha kwa viwango vya juu manunuzi ya mafuta ya Urusi.

Taarifa zinabaini kuwa Rais wa Urusi Vladimir Putin na Waziri Mkuu wa India Narendra Modi walijadili hii leo kwa njia ya simu kuhusu Ukraine.

Kwa habari nyingine za ulimwengu, tazama chaneli yetu ya YouTube.