1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kuleba yupo Beijing kwa mazungumzo ya kumaliza vita

23 Julai 2024

Waziri wa mambo ya nje wa Ukraine, Dmytro Kuleba yuko China kwa mazungumzo kuhusu jinsi maafisa wa huko wanaweza kusaidia kumaliza vita na Urusi, ambayo uhusiano wake na Beijing umeimarika tangu mzozo huo uanze.

Dmytro Kuleba
Waziri wa mambo ya nje wa Ukraine, Dmytro Kuleba Picha: Gleb Garanich/REUTERS

China inajipambanua kama mshirika asiyegemea upande wowote katika vita hivyo na kusema haitoi usaidizi hatari kwa pande zote mbili, tofauti na Marekani na mataifa mengine ya Magharibi.

Kuleba kuelekea China kusaka suluhu ya mzozo wa Ukraine

Hata hivyo, kuongezeka kwa ushirikiano wake "usio na ukomo" na Urusi kumesababisha wanachama wa NATO kuiita China kuwa  "mwezeshaji madhubuti" wa vita vya Moscow, ambavyo serikali ya Beijing haijawahi kulaani.

Ziara ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Ukraine Dmytro Kuleba ya hadi Ijumaa ni ya kwanza tangu vita kuanza Februari 2022.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW