Waziri wa uchukuzi wa Tanzania ziarani Ujerumani
17 Septemba 2012Matangazo
Dr. Mwakiyembe jioni hii (17.09.2012) anatarajiwa kusaini makubaliano ya ushirikiano wa usafiri wa anga baina ya Shirika la Ndege la Tanzania ATCL na la Ujerumani Lufthansa na vilevile kuangalia uwezekano wa serikali ya Ujerumani kusaidia katika uboreshaji wa usafiri wa reli. Sudi Mnette alizungumza naye akiwa Berlin na kwanza alitaka ufafanuzi kuhusu lengo hasa la ziara hiyo.
(Kusikiliza mazungumzo bonyeza alama ya spika za masikioni hapo chini)
Mwandishi: Sudi Mnette
Mhariri: Mohammed Abdulrahman