UchumiUjerumani
Robert Habeck kufungua mkutano wa kibiashara Kenya
3 Desemba 2024Matangazo
Akiwa mjini Nairobi, Kenya Waziri huyo wa uchumi wa Ujerumani pia ameyatolea mwito mataifa ya bara hilo kutengeneza mazingira bora ya uwekezaji.Mkutano huo wa kilele unaofanyika kila baada ya miaka miwili umehudhuriwa pia na waziri mkuu wa Kenya Musalia Mudavadi.
Takriban wajumbe 800 kutoka mataifa 35 ya Afrika na Ujerumani wanashiriki mkutano huo muhimu wa kibiashara kwa Ujerumani katika bara la Afrika.
Ujerumani kufanya biashara ya nishati na Nigeria
Bara hilo ni muhimu kwa uchumi wa Ujerumani kutokana na kasi na mabadiliko yake ya kiuchumi. Bara la Afrika ni la pili kwa ukuaji wa kasi wa kiuchumi duniani baada ya bara la Asia.