Waziri wa Ulinzi Austin asitisha safari baada ya kulazwa
13 Februari 2024Taarifa hiyo ni baada ya mkuu wa Pentagon kulazwa kwenye kitengo cha wagonjwa mahututi na kulazimika kukabidhi majukumu yake kwa naibu wake.Alipaswa kuanza safari kwa ajili ya mkutano wa NATO wa Alhamis lakini pia Jumatano ashiriki mkutano wa kujadili namna ya kuisaidia Ukraine katika makabiliano yake na uvamizi wa Urusi.Austin, mwenye umri wa miaka 70, Jumapili alipelekwa katika Kituo cha Matibabu cha Kijeshi cha Walter Reed kwa dalili zinazoashiria kuwa ni tatizo la kibofu. Inaelezwa pia kiongozi huyo hakuuweka hadharani upasuaji wa tezi dume aliofanyiwa Desemba na baadae Januari kulazwa hospitalini kukabiliana na matatizo yaliotokana na upasuaji huo.Bado haijaweza kujulikana mara moja ni kwa muda gani Waziri Austin atasalia hospitalini, lakini amekabidhi majukumu yake kwa Naibu Waziri wa Ulinzi Kathleen Hicks.