1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waziri wa Ulinzi nchini Ujerumani ajiiuzulu.

16 Januari 2023

Waziri wa Ulinzi nchini Ujerumani Christine Lambrecht amejiuzulu baada ya kukabiliwa na ukosoaji na shinikizo kubwa kufuatia hatua zake kuelekea Ukraine.

Deutschland | Lambrecht zu Pannen beim Schützenpanzer Puma
Picha: Kay Nietfeld/dpa/picture alliance

Waziri wa huyo wa Ulinzi nchini Ujerumani Christine Lambrecht ametowa taarifa ya kujiuzulu leo Jumatatu akisema kwamba amewasilisha ombi lake hilo kwa Kansela Olaf Scholz na kuongeza kwamba miezi kadhaa ya kumulikwa kwake na vyombo vya habari kumeondowa mjadala wa kweli kuhusu jeshi na sera ya usalama ya Ujerumani. Waziri huyo wa ulinzi wa Ujerumani ambaye amekuwa akikosolewa kuhusu hatua zake kuelekea Ukraine amesema kazi muhimu ya wanajeshi na watu wengi kwenye wizara yake inapaswa kupewa kipaumbele. Hatua ya kujiuzulu Lambrecht imekuja katika kipindi nyeti ambacho Kansela Scholz anakabiliwa na shinikizo kubwa la kumtaka achukue hatua nyingine kubwa ya kuipatia msaada wa kijeshi  Ukraine.