Waziri wa ulinzi wa China Li Shangfu anazuru Urusi
14 Agosti 2023Waziri huyo wa ulinzi wa China ameondoka leo Jumatatu kuelekea katika ziara hiyo ya siku sita ambapo anatarajiwa kuhutubia katika mkutano kuhusu usalama wa Kimataifa na pia atakutana na viongozi wa ulinzi wa Urusi na mataifa mengine. Kwenye mkutano huo, waziri wa mambo ya nje wa Urusi Sergei Lavrov anatarajiwa kuzungumzia ajenda itakayojikita katika kile kinachoitwa nchi zenye idadi kubwa duniani kutafuta njia mbadala za maendeleo nje ya mifumo ya nchi za Kimagharibi. Wajumbe kutoka kiasi nchi 100 na mashirika manane ya kimataifa wamealikwa kushiriki kwenye mkutano huo. Kushiriki kwa waziri wa ulinzi wa China katika mkutano huo kunadhihirisha kiu ya China na Urusi ya ushirikiano wa sera zao za nje kwa lengo la kuhujumu mfumo wa demokrasia ya kiliberali inayoongozwa na nchi za Magharibi.