Ujerumani yahofia vita vya Ukraine kusambaa
19 Januari 2024Matangazo
Pistorius ameliambia gazeti la Ujerumani la Tagesspiegel kwamba wanasikia vitisho karibu kila siku kutoka Urusi na hasa kitisho cha hivi karibuni dhidi ya mataifa ya kanda ya Baltiki.
Waziri huyo wa ulinzi amesisitiza kuwa wanapaswa kuimarisha haraka uwezo wao wa ulinzi kwa kuzingatia vitisho hivyo.
Pistorius amesema wanapaswa kuzingatia kwamba Rais wa Urusi Vladmir Putin anaweza siku moja kuzishambulia nchi za Jumuiya ya Kujihami ya NATO.
Amebainisha kuwa iwapo hilo litatokea, itakuwa kati ya miaka mitano hadi minane kuanzia sasa. Pistorius pia amekataa wito wa kuongeza msaada zaidi wa kijeshi wa Ujerumani kwenda Ukraine.