1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waziri wa zamani na mshirika wa Kabila akamatwa Kinshasa

17 Desemba 2025

Katibu mtendaji wa chama cha PPRD cha rais wa zamani wa Kongo, Joseph Kabila, Emmanuel Ramazani Shadary amekamatwa jijini Kinshasa.

Demokratische Republik Kongo | Bendera ya chama cha  PPRD
Taarifa ya chama cha PPRD imesema kukamatwa kwa Shadary na upekuzi wa usiku kwenye makao makuu ya chama kunatia wasiwasi.Picha: Bakoo/Afrikimages/IMAGO

Taarifa ya chama cha PPRD imesema kukamatwa kwa Shadary na upekuzi wa usiku kwenye makao makuu ya chama kunatia wasiwasi.

Kulingana na familia yake, Shadary, aliyewahi kuwa Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya Ndani na mgombea urais katika uchaguzi wa mwaka 2018, alikamatwa nyumbani kwake na watu wasiojulikana na hadi sasa hajulikani alipo.

Kukamatwa kwake kunatokea katika mazingira ya kisiasa yenye mvutano, takribani miezi mitatu baada ya kiongozi wa chama hicho na rais wa zamani Joseph Kabila kuhukumiwa adhabu ya kifo kwa makosa ya uhaini.