1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waziri wa zamani wa Rwanda kutumikia kifungo Senegal

21 Julai 2021

Waziri wa zamani wa Rwanda Augustin Ngirabatware, ambaye alihukumiwa kifungo cha miaka 30 gerezani kwa kuhusika na mauaji ya kimbari ya Rwanda, atatumikia kifungo chake kilichobaki nchini Senegal.

Augustin Ngirabatware Archiv
Picha: E.Ruguririza/AFP/GettyImages

Waziri wa zamani wa Rwanda Augustin Ngirabatware, ambaye alihukumiwa kifungo cha miaka 30 gerezani kwa kuhusika na mauaji ya kimbari ya Rwanda, atatumikia kifungo chake kilichobaki nchini Senegal.

Hayo yameelezwa leo na mawakili wake mjini The Hague.

Mei 28, Jaji Carmel Agius wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu, MICT alisema amemuelekeza msajili wa mahakama amuhamishie Ngirabatware nchini Senegal ili kutumikia adhabu yake.

Ngirabatware alikuwa waziri wa mipango wakati mauaji ya kimbari yanafanyika, ambapo Watusti 800,000 na Wahutu wachache waliuawa kati ya Aprili na Julai mwaka 1994.

Alihukumiwa Desemba mwaka 2012 kwa kuchochea, kusaidia na kuwahamasisha wapiganaji wa Kihutu katika wilaya ya Nyamyumba kaskazini magharibi mwa Rwanda kuwaua na kuwabaka majirani zao wa Kitutsi.

Hukumu ya awali ya miaka 35 jela ilipunguzwa hadi 30 mwaka 2014, baada ya kumuondolea kesi ya ubakaji.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW