1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaKorea Kusini

Waziri wa zamani wa ulinzi wa Korea Kusini akamatwa

9 Desemba 2024

Polisi wa Korea Kusini wamemkata Waziri wa zamani wa ulinzi wa nchi hiyo Kim Yong-hyun, huku kukiwa na uchunguzi wa madai ya uhaini.

Waziri wa zamani wa ulinzi wa Korea Kusini Kim Yong-hyun
Waziri wa zamani wa ulinzi wa Korea Kusini Kim Yong-hyunPicha: Celal Gunes/Anadolu/picture alliance

Hatua ya kukamatwa kwa kiongozi huyo ni kutokana na jukumu lake katika sheria ya kijeshi iliyotangazwa na Rais Yoon Suk Yeol, ambaye amenusurika kuondolewa madarakani kwa kura ya kutokuwa na imani naye Bungeni.

Hata hivyo kiongozi wa chama kikuu cha upinzani huko Korea Kusini Lee Jae-myung, amesema chama hicho kitajaribu tena Desemba 14  kumuondoa madarakani rais Yoon Suk Yeol,  kufuatia hatua yake ya kutangaza sheria ya kijeshi.

Ripoti za vyombo vya habari nchini humo zinaeleza kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani Lee Sang Min, ambaye ni mshirika wa karibu

wa Rais Yoon Suk Yeol, amejiuzulu wakati mzozo wa kisiasa ukiendelea kufukuta nchini humo.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW