1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wazungu waliokolea kwanza katika shambulizi la Msumbiji

14 Mei 2021

Shirika la kimataifa la kutetea haki za binaadam, Amnesty International limedai katika ripoti yake kuwa timu za uokoaji zilitoa kipumbele kwa wazungu na mbwa wao juu ya watu weusi wakati wa operesheni ya uokozi Msumbiji.

Mosambik Palma | nach Angriff von Rebellen
Picha: Dave LePoidevin/MAF/AP/picture alliance

Katika ripoti hiyo iliyokusanywa baada ya mahojiano na manusura 11 weusi, imesema helikopta iliyotumika kuwaokoa manusura kutoka katika hoteli walimojificha iliwaokoa mbwa kabla ya watu weusi. Soma Amnesty yashutumu mauaji ya raia mzozo wa Msumbiji

Aidha ripoti ya Amnesty International inasema makandarasi wazungu walibebwa na helikopta hio kabla ya wenyeji weusi, na kuongeza kuwa meneja wa hoteli aliwabeba mbwa wake wawili aina ya German Shepherd ndani ya helikopta hio na kuwaacha watu nyuma. Soma zaidi Watu 180 wakwama hotelini Msumbiji baada ya shambulizi

Kampuni ya kibinafsi ya Dyck Advisory Group (DAG),iliyoajiriwa na serikali ya msumbiji kuisaidia serikali kupigana na wanamgambo ambayo pia ilifanikisha operesheni ya uokoaji imekanusha madai ya ripoti ya Armensty International. 

Mwanzilishi wa kampuni ya DAG kupitia ujumbe wa simu ameiambia AFP kuwa madai hayo ni ya uongo na akaahidi kutoa tamko rasmi baadaye.

Watu walijificha katika hoteli

Picha: Dyck Advisory Group/REUTERS

Wanamgambo wanaojiita dola la Kiislam IS waliuvamia mji huo wa pwani mnamo Machi 24, na karibu watu 200, haswa wafanyikazi wa umma na wageni wanaofanya kazi kwenye mradi wa gesi ulio karibu, walijificha katika hoteli ya Amarula Palma wakati wa shambulio hilo. Soma Mamia ya watu wauawa katika mashambulio ya wanamgambo nchini Msumbiji

Mkurugenzi wa kanda ya Mashariki na Kusini mwa Afrikan wa Shirika la Amnesty International anasema madai hayo ya kutisha yanaashiria kuwa uokoaji ulifaywa kibaguzi.

Manusura mmoja ameliambia shirika hilo la kutetea haki za binaadam kuwa hawakutaka wazungu wote waokolewe kwani walijua iwapo wazungu wote wangeondolewa basi watu weusi wangeliachwa wafe. 

Lakini manusura mmoja mzungu kutoka Africa Kusini Wesley Nel ambaye kakake aliuwawa wakati wa shambulizi hilo amekanusha madai ya kuwepo kwa ubaguzi wa rangi wakati wa operesheni ya uokoaji.

Wengine walikatwa vichwa

Picha: Dave LePoidevin/MAF/AP/picture alliance

Miili kumi na miwili iliyokatwa vichwa ilipatikana imetandazwa mbele ya hoteli siku chache baada ya shambulio hilo, kulingana na jeshi na vyanzo vya usalama vya kibinafsi. Soma Ureno yajiandaa kupeleka wanajeshi wake Msumbiji

Shambulio hilo liliashiria kuongezeka kwa nguvu katika uasi ambao umesababisha maafa kote katika mkoa wa Cabo Delgado kwa zaidi ya miaka mitatu wakati wanamgambo hao wakipambana kuanzisha utawala wa ukhalifa.

/AFP