1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ujerumani: visa viwili vipya vya virusi vya corona

26 Februari 2020

Ujerumani imetangaza visa viwili vya maambukizi mapya ya virusi vya corona, katika majimbo ya katika majimbo ya North Rhine-Westphalia na Baden-Württemberg.

Coronavirus - Virus Sars-CoV-2  COVID-19
Picha: Imago Images/Zuma/Cdc

Ujerumani imeripoti visa viwili vipya vya maambukizi ya virusi vya corona Jumatano, katika majimbo ya North Rhine-Westphalia na Baden-Württemberg. Mataifa mengine yapatayo matano barani Ulaya yametangaza visa vipya vya maambukizi vya watu waliotoka eneo la Lombardy nchini Italia.

Italia ni nchi iliyoathirika zaidi na maambukizi ya virusi hivyo nje ya mashariki mwa bara la Asia, ikiwa imeripoti zaidi ya visa 300 vya maambukizi hayo ya virusi vya corona.

Miji kadhaa katika eneo hilo la kaskazini mwa Italia imewekewa marufuku ya watu kutoka nje. Hapo jana Jumanne, Uswisi, Austria na Croatia pia zimethibitisha visa vya kwanza vya maambukizi ya virusi hivyo.

Hayo yanajiri siku moja baada ya Shirika la Afya Duniani (WHO) kuzitaka nchi zote kujitayarisha kukabiliana na mripuko wa virusi hivyo vya corona.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW