1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaColombia

Wenye kujihami kwa silaha wasajili watoto 190 Colombia

13 Februari 2024

Ripoti mpya ya Shirika la Haki za Binadamu la Colombia (DPC) inasema watoto 190 wakiwemo hadi wa umri wa miaka tisa na wengi wao kutoka jamii za kiasili, wameandikishwa kwa nguvu na makundi yenye silaha 2023.

Kolombia Bogota | Gustavo Petro
Rais wa Colombia Gustavo Petro wakati wa hafla ya kuwapandisha vyeo maafisa wa jeshi wa nchi hiyo Oktoba 2, 2023.Picha: Sebastian Barros/ZUMA/picture alliance

Shirika hilo limelaani kitendo hicho na kukiita "uhalifu wa kivita." Taarifa yake imesema jumla ya wavulana 110 na wasichana 74 walinyakuliwa kutoka katika familia zao, wengi wao wakiwa na umri wa miaka 14 hadi 17, lakini pia baadhi ni wanafunzi wa shule za msingi. Afisa mwandamizi wa shirika hilo, Carlos Camargo amekemea kitendo hicho akisema wasichana, wavulana na vijana wasibebeshwe silaha kwa kupiganishwa vita visivyo na maana ambavyo vimedumu kwa zaidi ya miaka 60 nchini humo.Duru za serikali ya Colombia zinaeleza kuwa kwa miongo sita ya makabiliano baina ya mgambo wa mrengo wa kulia, magenge ya dawa za kulevya na vikosi vya serikali kumesababisha kupotea kwa watoto 3, 198.