1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Werder Bremen iko katika hali ngumu ya kifedha

9 Oktoba 2020

Kocha wa Werder Bremen Florian Kohfeldt asema "hali ngumu ya kifedha" kilabuni humo katika ligi ya Bundesliga na wanapitia wakati mgumu kutafuta na kununua wachezaji kujaza pengo lililowachwa na mchezaji Davy Klassen.

1. Bundesliga |1. FSV Mainz 05 - Werder Bremen - Florian Kohfeldt
Picha: picture-alliance/Eibner-Pressefot /A. Neis

Davy Klassen amerudi katika timu yake ya zamani ya Ajax huko Amsterderm katika siku ya mwisho ya kipindi cha uhamisho siku ya jumatatu  kwa dau la euro milioni 11.

Bremen vile vile walitaka kumpiga bei Milot Rashica kuelekea Bayer Leverkusenlakini muda uliwapa kisogo na haikuwezekana.

"Tumeshindwa kufikia malengo yetu ya uhamisho kutoka kwa mtazamo wa kimichezo" alisema Kohfeldt.

Picha: Carmen Jaspersen/dpa/picture-alliance

Hii ni baada ya mechi ya krafiki shidi ya St.Pauli Hamburg Jumatano usiku.

"Werder Bremen iko katika hali ngumu ya kifedha. Kila mtu aelewe hilo, na kila mtu lazima apambane" aliongezea Kohfeldt.

Bremen ambao ni mabigwa wa zamani wa Bundesliga wameathirika kifedha kutokana na kuzuka kwa homa ya Covid-19 na waliponea kushuka daraja msimu uliopita.

Lakini bado klabu hicho kinapamabana na kimeanza msimu kwa ushindi wa mechi mbili kati ya mechi tatu walizocheza.