1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Werder Bremen wakaribia kurudi katika Bundesliga

25 Aprili 2022

Werder Bremen wameshika usukani wa Ligi ya daraja la pili Ujerumani baada ya kushinda mechi yao ya mwishoni mwa wiki dhidi ya Schalke 04 kwa mabao 4-1 na sasa wako kileleni kwa tofauti ya pointi moja.

DFB Cup - Semi Final - Werder Bremen vs. RB Leipzig (1 : 1)
Picha: Focke Strangmann/Getty Images

Bremen ndio wanaoongoza na pointi 57 huku Schalke wakiwa na pointi 56 na Darmstadt 98 ni ya tatu wakiwa na pointi 54.

Saint Pauli wanaishikilia nafasi ya nne na pointi 53 kisha hamburg wana pointi 51 katika nafasi ya tano kwa hiyo timu zote hizi zinapambana ili ziweze kupanda daraja na kushiriki Bundesliga msimu ujao.

Ikumbukwe kwamba timu mbili za kwanza zinapanda daraja moja kwa moja kisha ya tatu inacheza mechi ya mchujo na timu iliyomaliza ya tatu kutoka chini kwenye Bundesliga.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW