1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WFP imesitishja ugawaji chakula Yemen

5 Desemba 2023

Shirika la mpango wa chakula duniani,WFP, limesema limesitisha shughuli ya ugawaji chakula kaskazini mwa Yemen kutokana na upungufu wa fedha

Jemen Hilfe Katastrophenhilfe Flüchtlinge Flucht
Shirika la mpango wa chakula duniani WFP katika majukumu yake YemenPicha: AHMAD AL-BASHA/AFP/Getty Images

Sababu nyingnie ya hatua hiyo ni  kutoelewana na mamlaka ya eneo hilo kuhusiana na namna ya kuwashughulikia watu masikini huko. Shirika hilo la Umoja wa Mataifa  limesema uamuzi wake umechukuliwa baada ya kushauriana na wafadhili na umekuja baada ya mwaka mmoja wa mazungumzo na kushindwa kupatikanamakubaliano ya kupunguza idadi ya watu inaowasaidia kutoka milioni 9.5 hadi milioni 6.5. Akiba ya chakula katika maeneo  yanayodhibitiwa na Wahouthi inakaribia kabisa kumalizika na kurudisha msaada wa chakula katika eneo hilo huenda ikachukua  hadi miezi minne, kutokana na kuvurugika kwa mfumo wa usambazaji chakula. Mamilioni ya watu bado wanategemea moja kwa moja  msaada wa kibinadamu nchini Yemen.