1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroUkraine

WFP ina wasiwasi kuhusu usafirishaji nafaka Bahari Nyeusi

26 Juni 2023

Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula, WFP, limesema kutorefushwa kwa makubaliano ya kuruhusu usafirishaji nafaka kupitia bahari nyeusi, ni hatua itakayoliathiri kwa kiasi kikubwa eneo la pembe ya Afrika

Türkei I Getreidefrachter  auf Durchfahrt durch Bosporus
Picha: Chris McGrath/Getty Images

Afisa mwandamizi katika shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula,WFP, Dominique Ferreti amesema kutorefushwa kwa makubaliano ya kuruhusu usafirishaji nafaka kupitia bahari nyeusi, ni hatua itakayoliathiri kwa kiasi kikubwa eneo la pembe ya Afrika. Ameonya kwamba kupanda tena kwa gharama ya chakula kutaongeza idadi ya watu wanaokabiliwa na njaa ambayo imeshafikia mamilioni ya watu.

Serikali ya Urusi, mjini Moscow imetishia kujiondowa kwenye makubaliano hayo yanayofahamika kama ''mpango wa usafirishaji nafaka kupitia bahari nyeusi'' uliosimamiwa na  Umoja wa Mataifa na Uturuki, Julai mwaka jana.

Maafisa wa mashirika ya msaada wanasema kiasi watu milioni 60 bado wanahitaji msaada wa chakula katika nchi saba za Mashariki mwa Afrika na wanakhofia athari za kusitishwa kwa mpango huo.