1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroHaiti

WFP kuanza tena kupeleka msaada kwa ndege nchini Haiti

19 Novemba 2024

Huduma ya Umoja wa Mataifa ya kutoa misaada ya kibinaadamu kwa kutumia ndege itaanzisha upya safari zake nchini Haiti siku ya Jumatano.

Mfanyakazi wa Uwanja wa ndege nchini Haiti akipokea msaada wa Umoja wa Mataifa
Mfanyakazi wa Uwanja wa ndege nchini Haiti akipokea msaada wa Umoja wa MataifaPicha: JAIME RAZURI/AFP/Getty Images

Hii ni baada ya mapumziko ya wiki moja yaliyolenga kurekebisha masuala kadhaa ya kisheria na kiufundi. Hayo yameelezwa na Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) ambalo husimamia harakati hizo.

Umoja wa Mataifa ulisitisha Jumanne wiki iliyopita safari zake katika mji mkuu wa Haiti Port-au-Prince, siku moja baada ya  magenge ya wahalifu kushambulia kwa risasi ndege tatu za abiria na hivyo kupelekea mdhibiti wa usafiri wa anga wa Marekani kupiga marufuku kwa mashirika ya ndege kuruka katika anga ya taifa hilo la Caribbean linalokumbwa ghasia.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW