Usalama wa chakulaSudan
WFP kupunguza mgawo wa chakula Sudan kuanzia Januari 2026
12 Desemba 2025
Matangazo
Mkurugenzi wa masuala ya Dharura wa WFP Ross Smith amewaambia waandishi wa habari nchini Geneva leo Ijumaa kwamba kuanzia mwezi Januari watapunguza mgawo kwa asilimia 70 kwa jamii zenye njaa na asilimia 50 kwa wale wanaokabiliwa na kitisho cha njaa.
Jamii katika eneo la Darfur zimekumbwa na njaa na utapiamlo kufuatia mzingiro wa RSF kwenye eneo la Al-Fashir uliodumu kwa miezi 18.
Vita vilivyozuka mwaka 2023 kati ya jeshi la Sudan na wanamgambo wa RSF vimesababisha kile ambacho Umoja wa Mataifa umekitaja kama mgogoro mbaya zaidi wa kibinaadamu duniani.