JamiiSyria
WFP kupunguza msaada wa chakula nchini Syria
14 Juni 2023Matangazo
Shirika hilo limesema mgogoro wa kifedha ambao haujawahi kushuhudiwa unalazimisha kupunguzwa msaada kwa watu milioni 2.5 kati ya watu milioni 5.5 wanaotegemea shirika hilo kwa mahitaji yao ya kimsingi ya chakula.
WFP imesema ikiwa itaendelea kutoa msaada kwa watu milioni 5.5, itakosa chakula kabisa cha kuwapa watu ifikapo Oktoba.
Soma pia: Antonio Guterres aunga mkono kupelekwa misaada nchini Syria
Taaarifa hiyo inatolewa wakati Umoja wa Ulaya leo hii ukijiandaa kuwa mwenyeji wa Mkutano wa saba wa huko mjini Brussels wenye kujikikata katika kusaidia hatma ya Syria na Kanda nzima.