JamiiSudan
WFP: Sudan kuwa "janga kubwa zaidi la njaa duniani"
6 Machi 2024Matangazo
Mkurugenzi Mtendaji wa WFP Cindy McCain amesema kwasasa, maisha ya mamilioni, amani na utulivu wa eneo zima ziko hatarini.
McCain ameongeza kuwa miaka 20 iliyopita, eneo la Darfur ndilo lililokuwa na mzozo mkubwa zaidi wa njaa duniani na dunia ilijotolea kulisaidia akimaanisha eneo kubwa la Magharibi mwa Sudan, lakini sasa ni watu wa Sudan waliosahaulika.
Soma pia: Umoja wa Mataifa waituhumu RSF kwa uhalifu wa kivita Darfur
Mkuu huyo wa WFP amesema kwasasa, shirika hilo haliwezi kufikia asilimia 90 ya wale wanaokabiliwa na viwango vya dharura vya njaa na kwamba ni asilimia tano tu ya idadi ya watu wa Sudan wanaoweza kupata mlo mmoja kwa siku.