WFP: Uhaba wa chakula wafikia kiwango cha hatari
16 Januari 2026
Shirika la Mpango wa Chakula Duniani, WFP, linasema machafuko yanayoendelea katika eneo hilo pamoja na kupungua kwa misaada ya kibinadamu vimesababisha janga kubwa la njaa.
WFP imeeleza kuwa imepunguza mgao wa chakula kutokana na ukosefu wa ufadhili, na kwamba katika msimu wa njaa unaotarajiwa kati ya Juni na Agosti 2026, mamilioni wataingia katika viwango vibaya zaidi vya uhaba wa chakula.
Takwimu zinaonyesha kuwa idadi ya watu walioko katika hali ya dharura imeongezeka maradufu tangu mwaka 2020, kufikia milioni tatu. Zaidi ya watu 15,000 katika maeneo maalum ya jimbo la Borno, kaskazini mashariki mwa Nigeria, wako katika hatari ya maafa, kiwango ambacho hakijawahi kufikiwa kwa miaka kumi.
Jimbo la Borno limekuwa kitovu cha uasi wa itikadi kali za Kiislamu tangu 2009, mzozo ambao umeua zaidi ya watu 40,000 na kuwahamisha takribani milioni.