WFP: Vita vya Iran vimeongeza njaa duniani
6 Juni 2026
Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) limeonya kuwa mamilioni ya watu wanakabiliwa na njaa kali kutokana na athari za vita vya Iran vilivyosababisha kupanda kwa bei za mafuta duniani.
Kwa mujibu wa shirika hilo, watu milioni 2.5 nchini Somalia, milioni 2.3 nchini Afghanistan, na milioni 1.3 nchini Sri Lanka wanapata ugumu wa kupata chakula cha kutosha.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa WFP, Carl Skau, amesema uhusiano kati ya bei za nishati na chakula ni mkubwa, huku watu wa nchi maskini tayari wakitumia fedha zao zote kununua chakula. Anasema bei za chakula zinapopanda, watu hulazimika kula chakula kidogo zaidi.
Shirika hilo pia limeonya kuwa hali inaweza kuwa mbaya zaidi katika miezi ijayo na limetoa wito kwa wafadhili kuongeza msaada wa kibinadamu, hasa kwa Somalia na Afghanistan na kuzitaja Sudan, Gaza, Lebanon ya kusini, Yemen na Haiti kama maeneo yenye njaa kali.