JamiiEthiopia
WFP yaanza kusambaza tena chakula Ethiopia
10 Oktoba 2023Matangazo
Shirika la Mpango wa Chula la Umoja wa Mataifa, WFP, limesema katika taarifa yake kwamba limeanza tena kusambaza chakula kwa wakimbizi wapatao 900,000 kote nchini Ethiopia baada ya kuimarisha utaritibu wa udhibiti kufuatia ripoti za wizi mkubwa wa misaada yake.
Shirika WFP lilisitisha usambazaji wa msaada wa chakula kote nchini Ethiopia mnamo mwezi Juni mwaka huu baada ya Marekani kutangaza ilikuwa inasitisha utoaji kutokana na msaada kuelekezwa kwingine.
Shirika la WFP na Shirika la misaada la Marekani USAID hayakutoa taarifa za kina kuhusu kuibwa kwa misaada kulikosababisha maamuzi yao.