1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Usalama wa chakulaSyria

WFP yapunguza msaada wa chakula, Syria

13 Mei 2026

Umoja wa Mataifa umesema leo kwamba unapunguza msaada wa dharura wa chakula kwa Syria kwa asilimia 50 na kusitisha mpango wa ruzuku ya mkate ambao umesaidia mamilioni ya watu, kutokana na uhaba wa fedha.

Syria | Vifaa vya misaada katika ghala karibu na kivuko cha mpaka cha Bab al-Hawa
Shirika la Mfuko wa Chakula, WFP limesema limepunguza msaada wa chakula cha dharura nchini SyriaPicha: Omar Haj Kadour/AFP/Getty Images

Mkurugenzi wa Shirika la Mpango wa Chakula Duniani, WFP nchini Syria Marianne Ward amesema katika taarifa yake kwamba wanapunguza pia idadi ya watu wanaopatiwa msaada wa dharura kutoka milioni 1.3 hadi 650,000.

Shirika hilo limesema licha ya hali ya utulivu kurejea Syria tangu vita vya wenyewe kwa wenyewe vilipomalizika, lakini bado kuna watu milioni 7.2 wanaoteseka kutokana na uhaba mkubwa wa chakula.

Ward hata hivyo amesisitiza kuwa punguzo hilo la msaada limechochewa na vikwazo vya ufadhili na si kutokana na kupungua kwa mahitaji.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW