1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WFP yasimaisha mpango wa msaada wa chakula kwa muda Sudan

21 Desemba 2023

Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula ulimwenguni (WFP) limesitisha utoaji wa msaada wa chakula kwa muda katika baadhi ya maeneo ya jimbo la Gezira nchini Sudan.

 WFP
Nembo ya shirika la mpango wa chakula duniani WFPPicha: Million Hailesilassie/DW

WFP imesema katika taarifa yake kwamba mapigano yanaendelea kuenea katika maeneo ya kusini na mashariki mwa mji mkuu wa Sudan, Khartoum.

Takriban watu 300,000 wamelikimbia jimbo la Gezira katika muda wa siku chache, tangu mapigano yalipozuka mnamo wiki iliyopita.

WFP: Sudan hatarini kukumbwa na baa kubwa la njaa

Mkuregenzi wa WFP nchini Sudan Eddie Rowe, amesema licha ya shirika lake kusimamisha utoaji wa chakula katika baadhi ya maeneo kwenye jimbo la Gezira, lakini WFP inaendelea kutoa misaada wa chakula katika maeneo ambayo wafanyakazi wa shirika hilo wanaweza kuyafikia. 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW