1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroSudan

Msaada wa nadra wa chakula wawasili Sudan

23 Agosti 2024

Shirika la Mpango wa Chakula Duniani, WFP limetangaza kuwasili kwa msafara adimu wa misaada katika nchi ya Sudan iliyokumbwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Sudan Darfur El Fasher
Wanawake walioko kwenye makambi ya wakimbizi wa ndani nchini Sudan wakiwa wamepnga mstari kusubiri kupewa msaada wa chakula katika kambi ya Gadaref Mei 12, 2024.Picha: AFP

Misaada hiyo imefanikiwa kuingia Sudan kupitia kivuko cha mpaka kilichofunguliwa kwa muda na Chad.

Msemaji wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres, Stephane Dujarric, amesema zaidi ya malori kumi ya misaada yamevuka hadi Darfur kutoka Chad kupitia kivuko cha mpaka cha Adre.

Malori hayo ya shirika la WFP na Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM) yalikuwa yamebeba mtama, kunde, mafuta na mchele kwa ajili ya kuwasaidia takriban watu 13,000 wanaotishiwa na njaa katika eneo la Kereinik ,magharibi mwa Darfur.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW