1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Sheria na HakiAfrika

WFP yawachunguza maafisa wake kwa ulaghai Sudan

Hawa Bihoga
28 Agosti 2024

Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula WFP linawachunguza maafisa wake wawili wa ngazi za juu nchini Sudan kufuatia tuhuma za kadhaa ikiwemo ulaghai na kuficha taarifa kwa wafadhili.

Sudan | Helkopta ya WFP ikishusha misaada ya kiutu.
Helkopta ya shirika la WFP ikishusha msaadawa kiutu SudanPicha: Maciej Moskwa/NurPhoto/picture-alliance

Uchunguzi huo wa Ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa shirika hilo la mpango wa chakula WFP unafanyika katika wakati ambapo shirika hilo linaendelea kusaka ufadhili wa kukidhi chakula cha mamilioni ya watu nchini Sudan waliokimbia mapigano na kusababisha mzozo mbaya zaidi ulimwenguni.

Shirika la habari la Reuters limeripoti kuwa jopo la wachunguzi kumi na mopja watakuwa na jukumu la kuchukunguza iwapo maafisa hao wa WFP walitaka kuficha taarifa za jeshi la Sudan kuzuia misaada muhimu wakati wa vita hivyo vilivyodumu kwa miezi kumi na sita sasa dhidi ya wanamgambo was RSF wanaowania udhibiti.

Soma pia:Takriban watu 30 wauawa baada ya kuporomoka kwa bwawa, Sudan

Miongongini mwa wanaochunguzwa ni naibu mkurugenzi wa WFP nchini Sudan Khalid Osman ambaye alipangiwa majukumu ya muda nje ya Sudan, huku afisa wa pili akiwa ni Meneja wa WFP katika eneo hilo Mohammed Ali, akichunguzwa kwa tuhuma za kupotea kwa kiasi cha lita laki mbili za mafuta mali ya shirika hilo la Umoja wa Mataifa nchini Sudan. Hata hivyo, maafisa hao walikataa kuzungumzia shutuma hizo.

Vyanzo vya karibu ambavyo vinafuatilia uchunguzi huo vilisema naibu mkurugenzi wa WFP Osman anadaiwa kuwaficha wafadhili kwamba mamlaka zinazohusika na jeshi eneo la Port Sudan zilikataa kutoa kibali kwa malori 15 ya kubeba msaada wa kiutu yaliokuwa yakielekea Nyala kusini mwa jimbo la Darfur eneo ambalo linashuhudia idadi kubwa ya watu wanaohitaji msaada wa haraka. Malori hayo yalisubiri kwa takriban wiki saba kabla ya kupewa kibali cha kuendelea na safari.

Marekani yataka uchunguzi wa haraka

Shirika la Misaada la Marekani USAID ambalo ni mfadhili mkubwa wa WFP ikitoa takriban nusu ya michango inayohitajika na shirika hilo limeiambia shirika la habari Reuters kuwa lilitaarifiwa na WFP juu ya matukio yaliyotokewa mnamo Agost 20 ambayo yanaweza kuathiri oparesheni za WFP nchini Sudan, hatua ambayo USAID ilitaka uchunguzi wa mara moja.

Malori ya Shirika la WFP yaliobeba misaada ya kiutu kwa wakimbizi wa Sudan yakiwa yameegeshwa kandoni mwa barabara.Picha: ASHRAF SHAZLY/AFP

WFP na mashirika mengine ya Umoja wa Mataifa yamelalamika juu ya kushindwa kuyafikia maeneo ambayo yanauhitaji wa misaada ya kiutu, hasa katika maeneo yaliyo chini ya udhibiti wa RSF kama vile Khartoum na mikoa ya Darfur na Kordofan. Hata hivyo  mashirika hayo yalijiepusha na kuzilaumu pande zinazozozana.

Soma pia:Umoja wa Mataifa kuwawekea vikwazo makamanda wa RSF Sudan

Baadhi ya Wasudan wanasema bado hali ni mbaya, ikiwa ni pamoja na kukosekana kwa misaada muhimu ikiwemo chakula na dawa.

''Hakuna chakula, hakuma maji ya kunywa. Huduma za afya zilitolewa na madaktari wasio na mipaka kwa miezi mitatu ama minne na maji yalitolewa miezi miwili tu.''

WFP imekuwa ikikabiliana na hali ya njaa katika namna nyingi ambapo kwa sasa inatafuta kiasi cha dola bilioni 22.7 ili kuwafikia watu milioni 157 ikiwa ni pamoja na wengine milioni 1.3 wanaokabiliwa na njaa, wengi wao wakiwa Sudan na Gaza, lakini pia katika nchi kama vile Sudan Kusini na Mali.

Katika hatua nyingine Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linazingatia kuwawekea vikwazo majenerari wawili wa kikosi cha RSF, kwa kuhatarisha amani, usalama, na utulivu wa  Sudan kutokana na vita na ukiukwaji wa haki za binadamu unaoshuhudiwa nchini humo.

Ufafanuzi: Je ni nchi zipi zinahusishwa na vita vya Sudan?

01:48

This browser does not support the video element.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW