White House: Hatuna taarifa za mashambulizi ya Rafah
16 Machi 2024Marekani imesema hayo ikiwa ni saa chache baada ya ofisi ya Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu kusema kuwa imetia saini mipango ya operesheni hiyo ya kijeshi.
Kirby amewaambia waandishi wa habari katika Ikulu ya White House kwamba Marekani haitaunga mkono mpango huo bila ya mapendekezo "ya kuaminika" ya kuwalinda raia wa Gaza.
Zaidi ya watu milioni 1.5 wanajihifadhi katika mji huo wa kusini mwa Gaza, na washirika wa Israel kama Marekani wameonya dhidi ya operesheni ya haraka ya kijeshi katika mji huo ili kuwaondoa wapiganaji waliosalia wa Hamas walioko huko.
Rais wa Marekani Joe Biden amesema, kwa upande wake anaona uvamizi wa Rafah utavuka "mstari mwekundu" ikiwa hakutakuwa na mipango ya kuaminika ya kuwalinda raia.
Huku hayo yakiendelea, Meli ya kwanza ya chakula cha msaada iliyotokea Cyprus hadi Gaza jana Ijumaa imeanza kupakua shehena ya chakula katika eneo hilo la Palestina lililozingirwa.